1. Jumapili ijayo itakuwa ni Dominika ya kumi na sita ya kipindi cha kawaida, mwaka A. Tunawashukuru wote waliofanya huduma wiki hii. Wiki ijayo huduma zitakuwa kama ifuatavyo:
• Misa ya kwanza: saa 12:30 asub. –Mt. Martino Misa ya Nne: saa 5:30 asub– Wanakarama
• Misa ya Pili: saa 2:00 asub. – Senior Youth Misa ya Tano: saa 11: 30 jioni
• Misa ya Tatu: saa 3:30 asub. –Mt. Batholomew
2. Siku za watakatifu juma hili:
• Jumatano, tarehe 15/07/2026, Kumbukumbu ya Mt. Bonaventura, Askofu na Mwalimu wa Kanisa.
3. Mafundisho kwa ajili ya kipaimara ni kila Jumatatu na Alhamisi saa kumi na moja jioni kwa watoto, na saa kumi jioni kwa watu wazima.
4. Jumatatu ya tarehe kumi na tatu, mwezi wa saba, yaani kesho, itakuwa ni siku ya mchango kwa ajili ya ujenzi wa Grotto. Baada ya Misa ya jioni, tutasali rozari kwanza kisha baada ya rozari mchango utafanyika. Kila mmoja anaombwa kuchukua bahasha na kutoa kile alichojaliwa.
5. Usajili wa wanandoa bila malipo, kwa ajili ya seminaa ya tarehe 6 hadi 8 mwezi wa nane umeanza. Usajili huu unafanyika kupitia kwa waandishi wa majumuia, mashirika na makundi mbalimbali ya hapa parokiani.
6. Waliochukua bahasha za Mt. Vincent wa Paulo hapo awali, wanaombwa kuziweka kwenye boksi lao hapo karibu na ubao wa matangazo ama katika ofisi ya parokia.
7. Jumuia zote zitakutana leo kwenye ukumbi wa Roho Mtakatifu saa tisa kamili. Sote tunaombwa kuzingatia mda. Wanaliturjia wote wanaombwa kufika saa nane na robo kwa mipangilio ya ukumbi.
8. Mchango kwa ajili ya maendeleo ya kanisa, mwezi wa nane, utaongozwa na wanaume hivyo wanaume wote wanaombwa kujiandaa vilivyo, ili kuufanikisha mchango huo.
9. Kongamano la wiki ya neema, yaani Crusade, litaanza tarehe tisa mwezi wa nane na kuisha tarehe kumi na sita mwezi wa nane. Tusambaze habari hizi kwa wengine.
10. Kwaya ya Mt Pio wa Kumi wanawaomba wakristo wakautazame wimbo wao mpya kwenye YouTube channel yao ya (St Pius X choir_Kongowea).Wanaombwa kusubscrbe lakini pia wausambaze kwenye mitandao mingine ya kijamii.



